top of page

Karibu Jumatatu!

  • Jul 27, 2015
  • 2 min read

“ ukiona comrade anaenda mbio… nafasi inatafutwa kwa Mama Chella”

Jumapili sasa imekuwa zaidi ya maombi, kufua na kuibiana nguo, kuchoma kunguni na kutembeleana. Imekuwa siku ya kufunga pasipo na hiari. Kushinda kitandani bila mazungumzo.

Nakupenda Jumatatu. Ni heri hukuwa Jumapili niliposhambuliwa na watoto wa kunguni wakati ambapo nilijaribu kuzidisha usingizi. Waliniuma kwa ustadi. Wanauma kuliko mama yao. Sitaki Jumapili, siku ambapo wezi waliobobea hunyemelea na kupotea na nguo zetu tulizoanika. Hata vitambaa vya mkono. Sikuambii kwamba hata “zile za ndani” usipoziweka vizuri…

Walahi sipendi Jumanne. Ati mimi niende tena “mess” kula vipande vitatu vya nyama, supu sahani nzima kwa sima, ati shilingi sijui thelathini! Afadhali nihepe mhadhara (lecture) niunde vitumbua(pancake).

Jumatano usirudi tena! Ukirudi, tafadhali usirudi na huyu jirani yangu anayecheza “kanungo” mapema kuniamsha toka kwenye lepe langu zito. Mwambie Jumatano ijayo apunguze sauti, la sivyo nami nifungue “Mugithi”. Umnyamazishe huyu jirani anayeimba kwa sauti saa kumi na mbili kila anapooga kwa kuogopa maji. Naye asiniamshe.

Alhamisi sikutaki! Siku hii ambapo nauziwa maji yaliyochanganywa na unga wa ngano ati ni maziwa. Ishindwe! Ukirudi uwakomeshe. Au sivyo mimi Alhamisi ijayo hainipati ng’o! labda nirudi Ijumaa.

Ijumaa nakusubiri. Nataka sana kuona buibui mapema siku hiyo. Napenda kuchungulia wanaorauka mapema kwenda kusoma wakati ningali kitandani. Ni furaha zaidi kusikia mhadhiri akipiga simu kuomba hudhuru kwamba hataweza kufika chuoni.

Ijumaa, karibu tena. Jioni nisikie mitambo ikicheza LH1. Hapo najua umefika. Nitavaa vulana mbio mbio na kuelekea “stage”. Nipate mboga kiasi maradufu cha kile ninachouziwa Soweto. Afadhali ijumaa. Lakini Jumapili…

Nikae tena masaa kumi na mawili bila kula wala kunywa maji? Afadhali nibaki Jumamosi. Lakini hatima yako ilinifurahisha Jumapili. Baada ya muda mrefu wa kimya na kushinda kitandani, mara ghafla sauti na maneno yenye vicheko vilisikika; “ zimerudiiiii…!” mtu wa kwanza kasikika. “Naenda kunywa chai J.” Sauti ya pili ikajibu.

Lakini Jumapili… Waah!!

 
 
 

Comments


Featured Posts
Recent Posts
Archive
Follow Us
  • Facebook Basic Square
  • Twitter Basic Square
  • Google+ Basic Square
Search By Tags
  • Facebook - Black Circle
  • Twitter - Black Circle
  • Google+ - Black Circle

Also Featured In

© 2015 by The Legacy Publication. Created with Wix.com

bottom of page